Thursday, 24 October 2013

Kitendawili katika Afrika ya Mashariki

Niliskia kuhusu kitendawili baada rafiki yangu aliniambia kwamba Raila Odinga alitumia kitendawili akienda kuongea na umma. Rafiki yangu alicheka kwa sababu Raila alitumia kitendawili kueleza kulikuwa wasiasa wabaya sana - wasiasa ambao ni tofauti kati ya ndani na nje, kama mayai. Kuongea juu ya wasiasa kama hawa, alitumia "kitendawili".

Kitendawili ni nini? Kamusi yangu inaeleza kwamba kitendawili ni "riddle" kwa Kiingereza. Lakini ni tofauti kidogo, sindiyo? Baadhi ya "riddles" ni hadithi ya ajabu; hadithi na fumbo. Nani aliua nani? Au, yeye alitoroka jengo lile vipi?

Kitendawili ni kitu flani zaidi. Kamusi ya Kiswahili inandika kwamba ni "ki-tenda-wili", kama kutenda mara mbili. Huu ni mfano:

Kitendawili: Nyumba yangu kubwa, haina taa.

Jibu: Kaburi.

Watu wana akili sana. Kwa hivyo tunaweza kuwaza na kupanga maneno kusema vitu tofauti kwa sauti moja. Kama hii tunatenda mara mbili.

Hii ni vizuri lakini pia kuna tatizo flani moja.

Kwenye uchaguzi ya Kenya, tumeumwa kwa "kusema kwa chuki" ("hate speech"). Hili ni tatizo kubwa tukitumia intaneti. Kupiga tatizo hili, siku hizi watu wanajaribu kufundisha kompyuta kutafuta maneno ya chuki kuwaambia polisi. Ni kusaidia kusimama mapigiano kati ya makabili tofauti. Kama tumeona, hii haitashinda kabisa kwa sababu desturi ya kitenda-wili ina janja zaidi...